Search Open Account Branches Zakat Calculator Amana Bank Mtaani Facebook Instagram Linkedin

 

Amana Bank na Property International Katika Uwezeshaji wa Viwanja

Posted on: Nov 28, 18 | News

Amana Bank Ltd na Property International Ltd (PIL) inayofuraha kubwa ya kutimiza miaka mitatu ya kufanya biashara pamoja kutimiza ndoto ya watanzania kwa kuwawezesha kumiliki viwanja katika maeneo salama yaliyopimwa na kupata hati miliki.

Aidha Bw.Rajab amesema kuwa, Katika mkopo huo watu wengi wameweza kunufaika kutumia viwanja hivyo kupata mkopo kupitia benki hiyo ili kuwezesha kuinua uchumi na kukuza biashara zao.

"Mteja anatakiwa atangulize asilimia 20 ya thamani ya kiwanja kama malipo ya awali na kulipa kiasi kilichobaki kwa muda uziodi mwaka mmoja na nusu ila kwa sasa tumeongeza hadi miaka mitatu,"amesema Rajab.

Amana Bank kutokana na kuwajali wateja tumeongeza muda wa malipo kutoka mwaka mmoja na nusu hadi miaka mitatu na kuwapunguzia faida toka asilimia 14 hadi asilimia 12 kwa mwaka mmoja.

Bw. Rajab ameeleza kuwa kuelekea Wiki ya huduma kwa wateja itakayoanza Novemba 19 mwaka huu, wateja watapata fursa ya kununua viwanja kwa punguzo maalum la bei na kutakuwa na mwakilishi kutoka PIL ndani ya wiki nzima ya huduma kwa wateja katika matawi yote Jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Biashara wa Benki ya Amana, Munir Rajab amesema katika kipindi cha miaka mitatu wamefanikiwa kuwawezesha wateja zaidi ya 300 kumiliki viwanja vyao na kupatiwa hati halali.

Afisa Mkuu Mwendeshaji wa Kampuni ya Property International (PIL), George Obado amesema kuwa wameweza kushirikiana na Benki ya Amana na kufanikisha watanzania wengi kupata viwanja vilivyopimwa pia wamekuwa wanafanya marekebisho ya barabara kwa kiwango cha Changarawe ili kufika kwenye maeneo yaliyo na viwanja.

Obado amesema, mbali na hilo kwa sasa viwanja vipo katika miradi ya Kimbiji Sea View Kigamboni, Magodani Mkuranga, Mapinduzi Residence, Chekeni Farm Mwasonga -Tundwi, Fukayose Residence Barabara ya Bagamoyo -Msata, The Dar es Salaam Automobile Zone (DAZ), Riverside Residence, Coco Palm, Royal Palm Mwasonga, African Palm Estate na Dege Residence.

Mkuu wa Idara ya Biashara Amana Bank Bw. Munir Rajab akikabidhi rasmi hati ya kiwanja kwa Bi. Aisha Sifana katika hafla ya kutimiza miaka mitatu ya kufanya biashara pamojaAmana Bank na Property International Limited.

 

Bw. George Obado Afisa Muendeshaji Mkuu Property International Limited akikabidhi rasmi hati ya kiwanja kwa Bw. Stephano Mathias katika hafla ya kutimiza miaka mitatu ya kufanya biashara pamojaAmana Bank na Property International Limited.

 

 

 

 

x

Download Amana Bank App here →
appstore playstore