Search Open Account Branches Zakat Calculator Amana Bank Mtaani Facebook Instagram Linkedin

 

Amana Bank na USAID kutoa mitaji ya biashara kwa Watanzania.

Posted on: Nov 01, 19 | News

Mkurugenzi Mtendaji,Amana Bank Dk Muhsin Masoud katika picha ya pamoja wakionesha mikata baada ya kusaini na Dk. Diana B. Putman, Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika.

Dar es Salaam: Oktoba 7, 2019, Serikali ya Marekani, kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID), imesaini mkataba wenye thamani ya Dola za Kimarekani milioni 10 na Amana Bank.  Lengo la DCA ni kuimarisha uwezo wa benki  katika kutoa fedha kwa shughuli zinazohusiana na kilimo na biashara ndogondogo na za kati na kwa biashara zinazomilikiwa na wanawake na vijana nchini Tanzania.

Mkurugenzi Mtendaji,Amana Bank Dk Muhsin Masoud katika picha ya pamoja wakionesha mikata baada ya kusaini na Dk. Diana B. Putman, Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika.

 

Wakati wa hafla hii, Dk. Diana B. Putman, Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika alisema, “Mkataba huu umekusudia kuimarisha uwezo wa Benki ya Amana kutoa fedha kwa Kilimo biashara nchini Tanzania. Hivyo, tunatarajia utachangia katika ukuaji endelevu wa biashara zinazohusiana na kilimo.”

 Mbali na kufadhili upatikanaji wa mikopo, mkataba huu umeongeza upatikanaji kwa wateja na mikoa ya Tanzania, ikiwemo Zanzibar. Wakati USAID inashirikiana na benki za Kiislamu katika maeneo mengine duniani, mkataba na Amana Bank ni wa kwanza kwa Benki ya Kiislamu Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Dk. Diana B. Putman, Naibu Mkurugenzi wa USAID katika Idara ya Afrika (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji,Amana Bank Dk Muhsin Masoud (kulia)  wakitia saini Mkataba wa Dhamana wenye thamani ya Dola za kimarekani milioni 10 na Amana Bank

Dk Muhsin Masoud, Mkurugenzi Mtendaji, Amana Bank alisema, “Mara nyingi mtaji hutajwa kama sababu kuu inayorudisha nyuma ukuaji wa biashara katika sekta ya kilimo hasa katika biashara ambazo zinazomilikiwa na wanawake na vijana katika nchi nyingi zinazoendelea. Vizuizi vikuu ni pamoja na ukosefu wa umiliki wa dhamana, kwani kwa sehemu kubwa mila na desturi hazijazingatia haki ya mwanamke katika kumiliki mali, vilevile kukosekana kwa historia ya ukopaji na marejesho. Hivyo basi makubaliano haya, yataenda kusaidia kupunguza changamoto hizi”

Mkurugenzi Mtendaji,Amana Bank Dk Muhsin Masoud akizungumza na wageni waliofika kushudia makubaliano kati ya Amana Bank na USAID

Serikali ya Marekani na Amana Bank kwa jumla tunaunga mkono maendeleo ya biashara na mchango wa sekta binafsi katika kuchangia maendeleo ya Tanzania na uwezo wa kufikia hadhi ya kujitegemea.

Mkurugenzi Mtendaji,Amana Bank Dk Muhsin Masoud na Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID) Andy Karas wakizungumza na waandishi wa habari waliofika kushuhudia makubaliano kati ya Amana Bank na USAID

 

Mkurugenzi Mtendaji,Amana Bank Dk Muhsin Masoud na Dk. Diana B. Putman, Naibu Mkurugenzi wa USAID Idara ya Afrika katika picha ya pamoja na wateja wa Amana Bank walioanza kunufaika kibiashara na mradi wa USAID kupitia Amana Bank.

x

Download Amana Bank App here →
appstore playstore